Zidane ni mmoja kati ya makocha nguli Dunia, awapongeza wachezaji wake kwa ushindi mnono

Pamoja na Jose Mourinho na Pep Guardiola, Zidane amekuwa sawa na meneja wa Liverpool Bob Paisley na carlo Ancelotti , mtu ambaye alikuwa akifanya nae kazi kama msaidizi.
Zinedine Zidane kocha wa Real Madrid
"Ningependa kuwapongeza wachezaji kwa kuwa si rahisi kile walichofanya," Zidane alisema baada ya mchezo katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev.
"Hii ndio kazi. Hakuna maneno kuweza kuieleza. Hicho ndio kikosi hiki kilivyo. Hawana ukomo wa kile wanachoweza kufanya." Zidane alisema.
Zidane hakutaka kuchukua sifa nyingi baada ya kushuhudia kikosi chake kikipata ubingwa wake wa nne katika misimu mitano, na taji la 13 katika historia ya klabu hiyo katika kombe la Ulaya.
Post a Comment