Header Ads

BannerFans.com

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUUA MKE NA WATOTO WAKE 2 KISHA KUWATUMBUKIZA NDANI YA KISIMA CHA MAJI

Mahakama kuu    Kanda ya  Sumbawanga   imemuhukumu   Yustine   Robarti    32  Mkazi  wa   Kijiji  cha    Maji   Moto   Wilaya  ya  Mlele   Mkoa  wa   Katavi   kunyongwa  hadi  kufa   baada  ya  kapatikana  na   hatia ya   kumuua    mke  wake  na   watoto wake wadogo  wawili  na  kisha  kuwatumbukiza  ndani ya kisima  cha   maji .
  Hukumu   hiyo  ilitolewa  hapo  jana  na   Jaji wa  Mahakama kuu    Kanda ya  Sumbawanga  Adam Mambi katika vikao vya Mahakam kuu vinavyoendelea kufanyika katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi  baada ya   Mahakama  kuridhika  na      ushahidi  uliotolewa     Mahakamani hapo  na  upande  wa  mashitaka  uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria mkuu wa serikali wa Mkoa wa Katavi  Achiles Mulisi                                 
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka  Mwanasheria mkuu wa serikali wa mkoa wa katavi alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo hapo Mach 23 mwaka 2015 majira ya saa 7 za usiku baada ya kutokea  ugomvi  baina yake na mke wake wakati wakiwa wamelala chumbani na watoto wao wadogo ambao na hoa aliwaua pia.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Yustini alimpiga mke wake aitwaye Monica Lwiche  mwenye umri wa miaka 25 na kisha baada ya kumuuwa alimtupia katika kisima cha maji na pia aliwauwa  watoto wake wawili Eliza Robert mwenye miaka mnne na Frank Robart mwenye miaka sita kwa lengo la kuvuruga ushahidi kwakuwa wakati akifanya kitendo hicho  watoto wake walikuwa wakishuhudia
Kabla ya kufanya tukio hilo mshtakiwa alikuwa ameisha toa kauli za vitisho  kuwa endapo mke wake atarudi nyumbani atafanya jambo litakalokuwa la kihistoria na ambalo halitasahaulika  kwa wakazi wa kata hiyo.
Mshtakiwa katika kesi hiyo alikuwa anatetewa na wakili Patrick Mwakyusa ambapo upande huo wa utetezi ulikuwa na mashahidi wawili mshtakiwa mwenyewe na Baba yake mzazi ambapo katika utetezi huo waliiomba mahakama imwachie huru kwani upande wa mashtaka umeshinda kudhibitisha kama kweli alitenda kosa hilo.
Pia upande huo wa utetezi  ulidai kuwa  upande wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha kuwa wakati anafanya mauaji hayo hakuna mtu yoyote aliyeshuhudia tendo hilo la kumuuwa mke wake na watoto na kuwatupia katika kisima cha maji.
Utetezi huo ulipingwa vikali na mwanasheria wa serikali Achiles Mulisi wa kile alichodai kuwa wakatika ugomvi huo unatokea  mwanzoni mama mwenye nyumba alikokuwa amepanga mshtakiwa  alishuhudia ugomvi huo na ushahidi wa  maneno ya vitisho aliyoyatoa mshtakiwa ni ushahidi tosha kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo na kitendo cha kuwaua watoto nwake wawili wanaojua kuongea na kumwacha  mdogo aliyeokotwa barabarani ni ushahidi tosha.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adam Mambi  aliiambia mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na utetezi Mahakama lazima iangalie mambo  matatu ambayo ni ushahidi wa mazingira,je upande wa mashtaka unadhibitisha na kama kweli  mshtakiwa amehusika katika mauaji hayo au la.
Hivyo aliieleza mahamakama kuwa kutokana na maswali hayo matatu ambayo mahakama ilihoji ilidhika na ushahidi uliotolewa na upande wa amshtaka na hivyo kumtia hatiani mshtakiwa Yustin Robert kwa kosa la kifungu cha sheria namna 196 na 197 cha kanuni ya adhabu na alitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kabla ya kusoma hukumu.
Wakili wa mshatakiwa Patrick Mwakyusa allambia mahakama kutona na mshtakiwa kupatikana  na kosa chini ya kifungu hicho cha sheria ambayo adhabu yake ni nmoja tu hana kiti chochote cha kuiomba mahakama .
Naye Mwasheria wa serikali aliiomba mahakama itoe adhabu kali li iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na hasa wanaowauwa watu wasikuwa na hatia na kutokana na mauaji kuwa mengi mkoani katavi hasa kwa wanawake ni vyema mahakama ikatoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo
Baada ya maelezo hayo Jaji Adam Mambi alisoma kuhumu na kuieleza mahakama kuwa mshtakiwa Yustini amepatikana na hati ya kuuwa watu watatu hivyo Mahakam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa.

No comments

Powered by Blogger.