RIPORTI: kumbe urusi ndio iliidungua ndege ya Malaysia

Wajumbe wa ujumbe maalum
wa uchunguzi wa Ukraine wa shirika la ushirikiano na usalama barani
Ulaya-OSCE- wakikagua eneo ilipoanguka ndege MH17 Julai 2014
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesikitishwa na ripoti mpya kuhusu kutunguliwa kwa ndege ya abiria ya Malaysia MH17.
Ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi inasema kuwa ndege hiyo iliangushwa na kombora la Urusi katika anga ya Ukraine.
Hata hivyo Urusi imekanusha matokeo hayo ikisema ni ya upendeleo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitoa kauli yake kupitia msemaji wake, amesisitiza kuwa Baraza la Usalama katika azimio lake nambari 2166 la mwaka 2014, lilitaka mataifa yote kushirikiana kikamilifu katika juhudi za kutafuta nani mhusika wa tukio hilo ili awajibishwe.
Ameongeza kuwa katika hali kama hiyo, kujua ukweli wa mambo ni muhimu mno ili kupata haki kwa waathiriwa na familia zao.
Ajali hiyo ilitokea Julai 17 mwaka 2014 huko Ukraine na abiria wote 298 pamoja na wafanya kazi walifariki dunia. Idadi kubwa ya abiria wa ndege hiyo walikuwa ni raia wa Uholanzi.
Ndege hiyo aina ya Boeng 777 ilikuwa katika safari ya kawaida ikielekea Kuala Lumpur, Malaysia ikitokea Amstedam, Uholanzi.
Tangu wakati huo haijukilani ni nani aliyehusika na ndio maana mwaka 2014 Umoja wa Mataifa, ulitaka ufanywe uchunguzi kujua nani alihusika.
Timu iliyofanya uchunguzi imeundwa na wajumbe kutoka Australia, Ubelgiji, Malaysia, Uholanzi pamoja na Ukraine.
Post a Comment