Mo Salah rasmi kushiriki kombe la dunia baada ya kupata matibabu
Mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah atashiriki katika
michuano ya kombe la dunia, baada ya daktari wa timu yake ya taifa
kusema matibabu yake hayatachukua zaidi ya wiki tatu. Misri inategemea
kumtumia mchezaji huyo katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Uruguay
tarehe 15 Juni.Awali mshambuliaji huyo hakuweza kuzungumza na wanahabari alipowasili nchini Hispania kwa matibabu ya bega lake. Salah alipata majeraha alipokuwa aking'ang'ania mpira na beki wa Real Madrid Sergio Ramos. Alilazimika kutolewa huku kukiwa na hofu kuwa hataweza kuichezea Misri katika fainali za kombe la dunia nchini Russia mwezi ujao. Shirikisho la soka nchini Misri lilithibitisha kwamba Salah yuko Valencia kwa matibabu ambapo ambaiko anaandamana na maofisa wa matibabu wa klabu ya Liverpool.
Post a Comment