Header Ads

BannerFans.com

Simba fc yaongoza kuwa na washiriki wengi katika tuzo za Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi

 

Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara inatarajiwakufanyika Juni 23 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kufanyika kwa tuzo hizo ni utaratibu ambao Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiwekea kila mwaka baada ya kumalizika ligi kutoa tuzo kwa waliofanya vizuri kwa kushirikiana na Wadhamini wakuu wa VPL Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Plc na msimu huu tutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet

Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, pia kunatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika kuboresha.

Katika tuzo ya Mchezaji  Bora Simba imeongoza kwa kuwa na wachezaji 7 msimuhu walio tajwa kushiriki katika kinyang'anyiro hiko ambao ni Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni,Shiza Kichuya Asante Kwasi ukutimu ya Yanga fc, na Azam fc wakiingiza wachezaji watano kila timu

No comments

Powered by Blogger.