Chanjo ya Ebola yaanza kutolewa DRC

Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo leo wameanzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.
WHO linasema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamkaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.Huenda watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza leo
Awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano.
Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016 katika Afrika ya magharibi watakaopewa chanjo hiyo ya majiribio.
Uchunguzi uliofanyiwa chanjo ya ugonjwa wa Ebola mwaka jana umebaini kuwa inaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kwa takriban mwaka mmoja.
Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500.
Post a Comment