Kenya ya pambana kutokomeza vijiko vya plastiki
Baada
ya kushiriki na kufanikisha mafanikio ya kampeni ya kutokomeza matumizi
ya mifuko ya plastiki nchini Kenya, mwanaharakati na mpiga picha nchini
humo James Waikibia amesema hivi sasa ameelekeza nguvu zake kwenye
kutokomeza matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na
kutupwa.
Bwana Waikibia katika mahojiano yake amesema amejikita kutokomeza matumizi ya vifaa hivyo nchini Kenya kwa kuwa
Bwana Waikibia ambaye anaendesha kampeni yake kwa kupiga picha zinazoonyesha madhara ya utupaji hovyo taka zikiwemo plastiki amesema anafahamu vita vya kutokomeza vifaa hivyo itakuwa ni ngumu lakini ni vyema kufahamu kinachotokea kutokana na utupaji holela wa vifaa hivyo.
PiaWikibia amesema Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu unapigia chepuo uhifadhi bora wa baharà na maziwa kama njia mojawapo ya kulinda viumbe vya majini na afya za walaji wa vitoweo.

Post a Comment