Hofu ya tanda UN na kinachoendelea Gaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres aliyeko ziarani
Austria amezungumzia mambo muhimu yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo
silaha za nyuklia na ghasia huko ukanda wa Gaza.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Kansela wa Austria Sebastian Kurz mjini Vienna, Bwana Guterres amesema ingawa kuna tishio la kuendeleza silaha za nyuklia na zile za kemikali..
Aidha Guterres amesema "wakati mwingine kuna habari n jema na ningependa kutaja moja ambayo inahusiana na tangazo la hivi karibuni la Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kuwa ina nia ya kufunga eneo la majaribio ya nyuklia huko Punggye-ri. Napenda kukaribisha na kusema kufunga kabisa eneo hilo itakuwa muhimu katika kujenga Imani na kuchangia katika juhudi za amani endelevu na ukaguzi wa kuthibitika wa kuondoa nyuklia rasi ya Korea.”
Na kuhusu ghasia zinazoendelea huko Ukanda wa Gaza baada ya Marekani kuhamishia rasmi hii leo ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda mji wa Yerusalem, Bwana Guterres amesema..
Guterresa mesema“Nina hofu kubwa leo kutokana na ripoti kuhusu kinachoendelea Gaza, tayari idadi kubwa ya watu wameuawa.”
Kuhusu Austria ambayo kesho inaadhimisha miaka 63 tangu ipate uhuru na mamlaka kamili, Katibu Mkuu amesifu uhusiano bora kati ya Umoja wa Mataifa na taifa hilo hususan mchango wake katika kumairisha amani na usalama duniani.

Post a Comment