Seneta McCain akiri Marekani ilifanya kosa kubwa kuivamia Iraq kijeshi

John McCain, seneta mwenye misimamo mikali amekiri japo kwa kuchelewa kuwa Marekani ilifanya makosa kuanzisha vita vya kuivamia kijeshi Iraq mwaka 2003.
Kwa mujibu wa tovuti ya Politiko, McCain amekiri kupitia kumbukumbu zake zilizochapishwa hivi karibuni kuwa vita dhidi ya Iraq vilikuwa ni makosa; na yeye mwenyewe anabeba sehemu ya lawama kuhusiana na jambo hilo.
McCain ambaye alikuwa mmoja wa waungaji mkono wakubwa wa vita na uvamizi wa kijeshi dhidi ya Iraq ameongeza kuwa: "hakuna jina jengine vinaloweza kupewa vita vya Iraq ghairi ya "kosa kubwa" na hakuna shaka inapasa nibebe sehemu ya lawama hizo
Post a Comment