Header Ads

BannerFans.com

Waziri wa Denmark atoa matamshi ya utata dhidi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Waziri wa Uhajiri wa Denmark atoa matamshi ya kuuvunjia heshima mwezi mtukufu wa RamadhaniWaziri wa Uhajiri, Mshikamano na Maskini wa Denmark ametoa matamshi yasio ridhisha dhidi ya Uislamu kwa kuwataka Waislamu wa nchi hiyo wanapoanza kufunga na katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wachukue likizo makazini akidai kwamba amali za mwezi huo ni "hatari" kwa watu wote nchini humo.

Inger Stewart Berg, ambaye ni mwanasiasa mwenye mitazamo tofauti dhidi ya wahajiri na Uislamu alitoa matamshi hayo  dhidi ya Uislamu hapo jana katika kipindi hiki cha Saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 Katika makala aliyoandika katika jarida la BT, Bi Berg amewataka Waislamu wote wachukue likizo makazini mwao wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuepusha kile alichodai kuwa ni athari hasi kwa watu waliosalia katika jamii ya Denmark

 Waziri huyo  aidha amedai kwamba anahofia taswira hasi za Saumu kwa "usalama na uzalishaji"

"Chukulia mfano wa dereva ambaye hajanywa wala haja chochote kwa zaidi ya masaa 10, hii inaweza kusababisha hatari kwetu sote", amedai waziri huyo.

Huko nyuma pia, katika hatua ovu aliyochukua kwa kisingizio cha kutetea uhuru wa maoni, Inger Stewart Berg aliweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook picha ya katuni iliyochorwa na gazeti moja la Denmark katika mwaka 2006 ya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW. Kitendo hicho cha kishenzi cha Berg kiliamsha hasira za Waislamu wa nchi hiyo

No comments

Powered by Blogger.