Header Ads

BannerFans.com

Jamii Forum wafunga huduma Tanzania

JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Jukwaa maarufu nchini Tanzania Jamii Forums limekuwa miongoni mwa watoaji huduma za maudhui mtandaoni ambao wameathiriwa na kuanza kutekelezwa kwa sheria mpya za mtandaoni.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imewataka watu ambao wamekuwa wakitoa imetoa ilani kwa wahudumu wote ambao bado hawajapata leseni kukoma kutoa huduma hizo kuanzia leo.

Mamlaka hiyo imesema wahudumu hao wana hadi Ijumaa wiki hii kuhakikisha wamejipatia leseni la sivyo watachukuliwa hatua.

TCRA imesema wanaoathirika ni wamiliki wote wa blogu, majukwaa ya mitandaoni, redio na televisheni.
 Ujumbe wa Twitter wa @JamiiForums: TCRA  Ni kosa kisheria kutoa huduma ya maudhui ya mtandaoni bila kuwa na leseni. Kuanzia Juni 11, 2018 watoa maudhui hawaruhusiwi kuweka jambo/taarifa(post) mtandaoni! #JFLeo
Wameandika kwenye mtandao wao:

"Kutokana na notisi iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo Juni 10, 2018 inayotoa muda mfupi wa kututaka kusitisha utoaji huduma mara kabla ya Juni 11, 2018, tunalazimika kutii mamlaka na hivyo huduma hii haitapatikana kwa muda wakati tukifanya jitihada za kuhakikisha huduma inarejea.

"Kwa wateja wetu walio nchi nyingine, huduma hii itarejea mapema zaidi lakini kwa walio Tanzania kurejea kwa huduma kutategemeana na matokeo ya hatma ya jitihada za wawakilishi wetu walio Tanzania.

"Tunasikitika kuwa tunalazimika kufikia hatua hii ghafla lakini ni matumaini yetu kuwa wateja wetu mtaendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki."
Ujumbe wa mwisho kutoka kwa jukwaa hilo kwenye Twitter ulipakiwa usiku wa manane, na ulikuwa wa kutangaza taarifa hiyo kutoka kwa TCRA

Wanablogu ambao wataopatikana na hatia ya kutoheshimu sheria hizo mpya watakabiliwa na faini ya hadi milioni 5 ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama zote mbili kulingana na sheria hizo mpya, ilisema taarifa hiyo.

Mike Mushi, mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums alikuwa awali ameambia BBC kwamba kanuni hizo, ambazo zinawataka wachapishaji wa taarifa zenye maudhui mtandaoni kuhifadhi maelezo ya wachangiaji kwa miezi 12 huenda zikaathiri mtandao wa Jamii Forums.

"Sheria hizi zinaenda kinyume na jinsi sisi huendesha shughuli zetu. Huwa twawaruhusu watumiaji wetu kuandika ujumbe bila majina yao kutambulishwa, hivyo itatulazimu kufikiria kwa kina iwapo tutaweza kuendeleza kuendesha shughuli zetu."

Alisema mtandao huo kufikia Aprili ulikuwa na watumiaji 3.7 milioni kwa mwezi na walikuwa wanapokea ujumbe takriban 20,000 kila siku

No comments

Powered by Blogger.