SIMBA YA PINDUA MEZA KIBABE KWA MO IBRAHIM
KIUNGO mchezeshaji wa Simba anayesifika kwa mashuti ya mbali, Mohamed Ibrahim ‘Mo Ibra’ rasmi anasaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa dau la Sh. milioni 30 na kuachana na Yanga iliyokwisha muonyesha mkataba wa awali.MO ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusajiliwa na timu hiyo katika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na walishakubaliana mambo mengi kabla ya Simba kupindua meza kibabe.
Yanga ilitaka kumsajili huyo baada ya kupata taarifa za mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu uliomalizika wa ligi akiwa pamoja na Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin ambao tayari wameongezewa mikataba.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi, kiungo huyo amekubali kusaini kwa dau hilo la usajili baada ya kufikia muafaka mzuri na uongozi wa timu hiyo akitokea Morogoro kwa Basi.
Mtoa taarifa huyo ambaye Championi limejiridhisha
naye alisema, MO atasaini kwa dau hilo la usajili kwa mkataba wa miaka miwili huku akiboreshewa mshahara wake wa kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili ambacho atakachokuwepo Msimbazi.
“MO usajili wake umeshakamilika na kilichobaki ni yeye kuja kusaini mkataba pekee, kwani kila kitu tumekubaliana kwa maana ya dau la usajili na mshahara wake wa kila mwezi.
“Na tumekubaliana kwa pamoja kuwa atasaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 30 baada ya kufikia muafaka mzuri kati yetu viongozi na yeye mwenyewe mchezaji.
“Hivyo, MO hatakwenda tena Yanga kama ilivyokuwa inaelezwa na badala yake atabaki kuendelea kuichezea
Simba kwa miaka mingine miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa MO ambaye aliwahi kuzinguana na Kocha Pierre Lechantre aliyetimuliwa na Simba, alisema kuwa “Mkataba ni siri kati yangu mchezaji na viongozi, hivyo ni ngumu kwangu kuzungumzia makubaliano yaliyokuwepo katika mkataba wangu.
Post a Comment