DNA yazua kizazaa kwa Walimu wabakaji Kenya

Mwalimu mkuu katika shule ya upili
ya Moi Girls amewasilisha ombi kwa tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC,
kutaka kustaafu mapema baada ya tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika
shule hiyo mwishoni mwa juma ndani ya shule hiyo.
Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wakiume katika shule ya upili ya Moi Girls Nairobi wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa DNA wakati maafisa wa upelelezi wanajaribu kuchunguza tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa usiku.
Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa kiume wa walimu wanaoishi ndani ya Shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi.
Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumithilisha mshukiwa dhidi ya maji maji yanayopatikana katika mwili wa muathiriwa na hivyo kuweza kuwana ushahidi mzito katika kesi.
Itasaidia pia kubaini iwapo washukiwa wataokaochunguzwa walikuwa katika eneo la tukio hilo la uhalifu au kuwaondoshea makosa yoyote.
Polisi wanajaribu kuchunguza matukio yaliojiri usiku huo wa mkasa na siku ya pili iliyofuata kujua ukweli upo wapi katika tuhuma hizo za kubakwa kwa wanafunzi wa Moi Girls ambazo zimezusha hasira kubwa nchini.
Maafisa wanachunguza pia tuhuma kwamba maafisa katika shule hiyo waliwaambia wanafunzi wajioshe na wanyamaze kuhusu kinachotuhumiwa kutokea
Post a Comment