Rais Putin yupo ziarani China

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili nchini China na kukutana na rais Xi Jinping katika ziara ya siku tatu inayonuiwa kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi kwa nchi hizo mbili.
Rais wa China Xi Jinping alimkaribisha rais Putin kwa gwaride la heshima katika ukumbi wa kitaifa mjini Beijing. Viongozi hao ambao wote hawakualikwa katika mkutano wa kilele wa mataifa saba yalioimara kiuchumi G7, utakaofanyika nchini Canada Ijumaa (08.06.18) na Jumamosi (09.06.18) wanatarajiwa kutia saini makubaliano ya kibiashara baadaye hii leo.
Badaa ya kukaribishwa rasmi nchini humo Putin alikutana pia na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang kabla ya kuwa na mazungumzo rasmi na rais Xi. Putin alimwambia Li kwamba biashara kati ya Urusi na China pamoja na mahusiano ya kiuchumi yamefana na wanatafuta sehemu nyengine ya ushirikiano.
Li kwa upande wake amesema biashara kati yao inatarajiwa kufikia dola bilioni 100 mwaka huu huku akisema kuwa China iko tayari kabisa kupanua ushirikiano katika Nyanja mpya ikiwa ni pamoja na nishati ya nyuklia.
Post a Comment