Mahakama yaamuru marekebisho kesi ya mbowe na vigogo wengine wa chadema

Dar es salaam. Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imeamuru
upande wa Mashtaka kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka yanaomkabili
mwenyekiti wa cha Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine nane wa chama hicho
Uamuzi huo umetolewa leo jumatatujuni 11,2018 na Hakimu
Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.
Baada ya kutoa uamuzi huo, wakili wa utetezi peter kibatala
alielezea mahakamani hapo kuwa
hawajaridhishwa na uamuzi huo na akawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.
Hakimu mashauri alitoa uamuzi huo baada ya kupitia
mapingamizi nane yaliyowasilishwa mahakamani hapo na kibatala na jeremiah
Mtobesya.
Kwa pamoja kesi hiyo, hakimu Mashauri alikubaliana na baadhi
ya hoja za upande wa utetezi kuwa katika shtaka la pili,tatu, nne, tano,sita na
saba yana upungufu wa kisheria na kuamuru upande wa mashtaka kufanya mabadiliko
katika hati ya mashataka.
Baada ya kutoa uamuzi huo, wakili kibatala aliieleza
mahakama kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huoo hivyo aliwasilisha taarifa ya
kusudio la kukata rufaa
Kibatala amedai kuwa wanakata rufaa kwa sababu wao
waliomba mashtaka hayo yafutwe lakini Mahakama
imeamua yafanyiwe marekebisho kwenye hati ya mashtaka.
Baada ya kibatala kueleza hayo, wakili waserikali, Paul Kadushi amedai kuwa huo ni uamuzi mdogo ambao hauwezi kumaliza
kesi na kwamba uamuzi huo hawawezi kuukatia rufaa. Kibatala amesisitiza kuwa
kwa kuwa Mahakam imeona mashtaka
hayo ni batili
Post a Comment