Pascal Wawa yuko mbioni kusaini Simba
Mchezaji huyo amewasili nchini jana kwa ajili ya kuja kukamilisha mazungumzo ya mwisho na klabu ya Simba kwa ajili ya kusaini mkataba.
Beki huyo ambaye alikuwa anaichezea Azam FC, aliondoka na kumtikia Sudan kukipiga katika klabu ya Al Merrikh inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Wawa ameonekana akiwa mazoezini wakati kikosi cha Simba kikijinoa kwenye Uwanja wa White Sand, Mbezi Beach, kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajiwa kuanza wiki hii jijini Dar es Salaam.
Ujio wa Wawa katika klabu ya wekundu hao wa Msimbazi ni mojawapo ya pendekezo la benchi la ufundi ambali hapo awali lilitoa ripoti ya kuhitaji kuongezeka kwa beki mmoja wa kimataifa
Post a Comment