uamuzi wa Zidane kuachia ngazi wa mkosesha amani Perez

''Uamuzi wake ulikuwa kama mlipuko wa bomu''
Aliondoka
kama vile alivyowasili na alivyohudumia miaka yake miwili na nusu
akipewa heshima kubwa. Uamuzi wa Zidane kuondoa katika klabu ya Real
Madrid siku tano baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda kombe lake la
tatu la vilabu bingwa mfululizo umewaacha mabingwa hao wa Uhispania na
kizaa-zaa.
Rais wa klabu hiyo Florentino Perez alishangazwa na uamuzi huo , ambao Zidane aliutoa katika mkutano na vyombo vya habari siiku ya Alhamisi na sasa maafisa wa ngazi za juu katika uwanja huo watalazimika kufanya kazi ya ziada kumtafuta na kumfichua kocha atakayemrithi raia huyo wa Ufaransa.
Vyombo vya habari vya Uhispania pia vilipigwa na butwaa.
Habari kutoka katika mtandao wa Marca zilisema alikishangaza chumba cha maandalizi kama ''mlipuko wa bomu'', huku gazeti la El Mundo likisema katika kichwa chake cha habari ''Real Madrid haijaamini kwamba kunaweza kuwa na nahodha bora katika jahazi hilo gumu''.
Hatahivyo BBC inaangazia sababu za Zidane kuondoka na maana yake kwa mabingwa hao wa Ulaya
Ni kweli kwamba habari za kujiuzulu kwake zilimshangaza rais wa klabu hiyo Florentino Perez ambaye alitumia wakati mwingi wa mkutano huo na vyombo vya habari akionekana kama mtu aliyekosa jawabu katika uso wake akijaribu kuamini kile alichokuwa akisikia.
Perez alitangaza kwamba Zidane alimwambia kuhusu uamuzi wake siku iliopita, huku naye {Zidane} akifichua kwamba mchezaji wa pekee aliyezungumza naye kuhusu uamuzi wake ni nahodha Sergio Ramos.
Zidane alikuwa wazi kuhusu sababu zake za kuondoka , akikiri kwamba hajui atakavyoisaidia timu hiyo kuibuka mshindi msimu ujao huku akisisitiza kuwa timu hiyo inahitaji damu mpya mbali na kuzungumzia kuhusu shinikizo kali na mahitaji katika wadhfa huo.
Hakusema ni lini aliamua kuchukua uamuzi huo, lakini kulikuwa na ishara kadhaa, wakati alipoulizwa kutaja wakati wake mgumu wakati wa kipndi chake cha ukufunzi , Zidane hakusita kusema kuwa kombe la Copa del Rey ambapo timu hiyo ilibanduliwa na Leganes mnamo mwezi Januari.
Na swali la mwisho lililomkabili kabla ya kuondoka katika mkutano huo na klabu hiyo huku akishangiliwa ni iwapo alidhani kwamba ulikuwa wakati mwafaka kuondoka katika klabu hiyo baada ya kushinda taji lake la tatu la vilabu bingwa.
Zidane alitabasamu na kujibu ''pengine , pengine ni kweli''
Post a Comment