Feisal Toto aitosa yanga aelekea Singida

Mchezaji wa klabu ya JKU, Feisal Salum, maarufu kama Fei Toto, amefunguka na kueleza kuwa anaweza akaelekea Singida United endapo viongozi wa klabu hizo mbili watafikia mwafaka.
Toto ambaye alikuwa anatajwa kujiunga na Yanga amesema kwa sasa viongozi wa JKU wanaendelea kuzungumza na Singida na pale mwafaka utakapofikiwa wakikubaliana ataweza kuondoka.
Kiungo huyo ameonekana kuwa na kipaji cha aina yake ndani ya JKu jambo ambalo limezivuta kwa karibu Yanga na Singida United kunyemelea saini yake.
Yanga nao inaelezwa wapo kwenye mazungumzo na JKU lakini Singida ndiyo wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kumsajili.
Kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha JKU wakati JKU ikicheza dhidi ya Vipers ya Uganda katika mchezo wa michuano ya KAGAME kwenye Uwanja wa Chamazi Complex na timu yake ikienda sare ya bao 1-1.
Post a Comment