Yanga yawania saini ya Nyosso
Wakati
vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara likiendelea, taarifa
zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga wako kwenye mchakato wa kupata saini ya
beki mkongwe wa Kagera Sugar, Juma Nyosso.
Nyosso aliyewahi kutamba na kikosi cha Simba miaka kadhaa nyuma ameingia katika rada za Yanga ili kuboresha safu yake ya ulinzi.
Yanga inaelezwa kuwa kwenye mazungumzo na Kagera pamoja na mchezaji ili kuweza kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ikiwa inatarajia kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC Julai 18 2018.
Mpaka sasa Yanga haijaweka wazi kwa asilimia 100 majina ya wachezaji waliowasajili tangu msimu wa 2017/18 umalizike, ingawa tetesi zinasema tayari imeshamalizana na mshambuliaji wake wa zamani, Mrisho Ngassa.
Ujio wa Nyosso katika kikosi cha Yanga unaweza kuongeza nguvu ambapo atakuwa anacheza sambamba na Kelvin Yondani ikiwa atasalia Yanga kwa kuwa uongozi una mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mwingine
Post a Comment