Roger federer ashuka kiwango cha tennis
Kutokana na kufungwa jana kwenye mechi ya fainali katika mashindano ya Halle ya Ujerumani, Roger Federer wa Uswisi anashuka kutoka nafasi yake ya kwanza ya viwango vya ubora wa tennis duniani, na nafasi hiyo inachukuliwa na Rafael Nadal wa Hispania.
Federer alifungwa na Borna Coric mwenye miaka 21 wa kutoka Croatia kwa seti yenye alama 7-6, 3-6 na 6-2 na kukatisha rekodi ya ushindi mfululizo mara 20 aliyokuwa nayo Federer, na huu ni ushindi wa kwanza kwa Coric dhidi ya wachezaji waliorodheshwa kwenye kumi bora duniani.
Federer sasa ataingia kwenye mashindano makubwa ya Wimbledon akiwa si namba moja kwa ubora kama ilivyotarajiwa.
Post a Comment