Baada ya kumpindua Mugabe,Mnangawgwa rasmi atua Dar es salaam jana

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa yuko Dar es salaam katika ziara ya kwanza nchini humo tangu aingie madarakani.
Ni ziara ya siku mbili ambayo imetajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyeji rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais Mnangagwa wamekubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili yaliotajwa kuwa na udugu wa kihistoria.
Mnangagwa amewasili asubuhi jana na kupokewa na rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akiwa Tanzania kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea miongoni mwa wapiganjiaji uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika.
Tanzania ilikuwa na jukumu muhimu katika mataifa ya Afrika yaliojikomboa dhidi ya utawala wa wazungu.
Makao makuu ya muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama (OAU), yalikuwa mjini Dar es Salaam ambapo mikakati iliidhinishwa kumegua utawala wa kikoloni katika nchi za Afrika.
Post a Comment