Nkurunziza amesema atang'atuka madarakani 2020
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametangaza kuwa ataondoka madarakani mwaka 2020 wakati muda wake wa urais wa sasa utakapomalizika.
Rais Nkurunziza aliyasema hayo baada ya kusaini na kutangaza katiba mpya katika mji wa Gitega, katikati mwa Burundi. Katiba mpya ya Burundi imeongeza muda wa urais kuwa miaka 7 kutoka mitano ya zamani, na kuruhusu rais kuchaguliwa kwa vipindi viwili mfululizo. Hii inamaanisha kuwa, rais Nkurunziza anaruhusiwa kuendelea kuwa madarakani hadi mwaka 2034 kama akichaguliwa katika chaguzi zijazo.
Post a Comment