Bingwa wa michezo ya Commonwealth Mita 800 Wycliffe Kinyamal leo
anateremka dimbani Rome Golden Gala nchini Italia, akitaka kuweka medali
nyingine kibindoni. Akiwa bado ana joto la ushindi wa michezo ya
Jumuiya ya madola mwezi uliopita, na ushindi wa diamond League mjini
Shanghai Mei 12, Kinyamal atatumia fursa ya leo kuondoa uchungu wa
kumaliza katika nafasi ya tatu jumamosi iliyopita huko Eugene Marekani.
Kinyamal pia alitimuliwa vumbi na mkenya mwenzake Emmanuel Korir
aliyepaa nafasi ya pili.
Post a Comment