Burundi ya piga kura ya maamuzi ya kuongeza muhula wa urais

Rais Nkurunziza amepiga kura yake kituoni ECOFO Buye, tarafani Mwumba, Mkoa wa Ngozi
Burundi inafanya kura ya maamuzi hapo inayopania kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba.
Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034.Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani.
Umoja wa mataifa unahofia huenda ghasia zikazuka baada ya mauaji ya watu 26 hivi majuzi.
Wiki jana, washambuliaji ambao serikali imewataja kuwa magaidi, walivamia jiji la Chibitoke, wakafanya mauaji ya kiholela na kuaminika kutorokea taifa jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali inaamini kuwa walikuwa wanajaribu kukomesha kura ya maoni kwa kutia watu woga na kuvuruga amani. Hali hii ikiendelea huenda warundi wengine wasipige kura. Ni kura tata yenye matokeo makubwa
Post a Comment