ABDU KIBA: skendo azina nafasi kwangu mimi
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdu Kiba, amesema maisha yake
ya muziki hayasukumwi na skendo za mitandao ya kijaami, badala yake
ataendelea kutumia kipaji chake na kutoa kazi zenye viwango.Akizungumza na MWENDA PLUS BLOG leo, Kiba alisema wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini.
“Muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu mimi na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndio maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu.
“Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake,” alisema Kiba.
Post a Comment