Kipa wa Liverpool awaomba msamaha mashabiki kwa uzembe alioufanya jana dhidi ya Madrid

Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius akitokwa na machozi baada ya makosa aliyofanya kuigharimu timu yake.
Mlinda mlango wa liverpool Mjerumani Loris Karius aliizawadia Real madrid bao la kuongoza katika dakika ya 51 wakati, alipojaribu kuharakisha kuanzisha mashambulizi, aliurusha mpira mbele ya mshambuliaji wa Real Karim Benzema, ambaye alinyoosha mguu wake na kuuweka mpira wavuni. karius , mwenye umri wa miaka 24 , pia alifanya makosa katika goli la tatu la Real wakati Gareth Bale alijaribu kupiga mpira ya mbali ambao ulijaa wavuni baada ya kumchoropoka kipa huyo wa Liverpool.
"Sijisikii kitu chochote sasa hivi. Leo nimesababisha timu yangu kupoteza mchezo na najisikia vibaya sana na nasikitika na kuomba msamaha kwa kila mtu," Karius alisema.
"Naomba samahani kwa kila mtu, kwa timu, kwa klabu , kwamba makosa hayo yameigharimu timu. Iwapo ningerudisha nyuma muda , ningeweza. Nina masikitiko makubwa kwa timu yangu. Nafahamu nimewaangusha leo.
"Magoli haya yametugharimu kukosa ushindi, kimsingi," aliongeza.
"Ni vigumu kwa sasa lakini hayo ndio maisha ya mlinda mlango. Unapaswa kuinua kichwa chako juu tena."
Post a Comment