SERIKALI YA POKEA VIFAA VYA UPASUAJI KUTOKA UBALOZI WA KUWAIT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsalimia mtoto Daniella Wilfred Pallangyo mwenye umri wa miaka 8 ambaye ana matatizo ya kichwa kikubwa wakati wa hafla ya kupokea
vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa
Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa(MOI)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI,
zitaipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo
kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya
kwa wananchi.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji
wa Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI) .“ Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru
Mheshimiwa Balozi wewe binafsi na Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano
ambao mnaendelea kuipatia Serikali yetu ya awamu ya Tano katika Sekta
mbalimbali za maendeleo lakini hasa hasa katika sekta ya afya”
alishukuru Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais amesema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa
mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo wamesaidia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo
vitaiwezesha Taasisi kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa
watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Makamu
wa Rais amesema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha
upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa
watakaopata huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi,
kufikia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka
zaidi

Post a Comment