Kumbe Azam fc imeipa ubingwa Simba fc msimu huu

Na mwenda plus
Msimu wa ligi kuu Tanzania bara2017/18 almaarufu VPL ukikaribia kufika ukingoni uku kila timu kwenye ligi hiyoo ikibakisha michezo michache na tayari bingwa wa ligi hiyoo ameshapatikana ambayo ni timu ya soka ya simba sport club ya jijini Dar es salaam almaarufu wekundu wa msimbazi wamechukua ubingwa huo kwa kujikusanyia zaidi ya alama 68 nyuma ya mahasimu wao Azam fc wakiwa na alama 55 kibindoni wakifatiwa na yanga fc wakiwa na alama 48 uku maji maji fc, ndanda fc na njombe mji zikiwa hatarini kuteremka daraja.
Baadhi ya wadau wa soka
wametoa maoni yao kuhusiana na
mwenendo wa ligi nzima na kupongeza mabingwa wa msimu huu ambao ni simba fc
kwakuonyesha kiwango kizuri cha soka na kupoteza mchezo mmoja tu hadi sasa. Licha ya kandanda
zuri walio onyesha pia simba msimu huu wamekua na kikosi bora kabisa kikiongozwa na mchezaji wa kimataifa kutokea Uganda Emanuel Okwi akiongoza kwa magoli 20 akifatiwa
na John Bocco akiwa na magoli 14.
Pia wadau wamezungumzia mbinu zilizopelekea Simba kupata
ubingwa msimu huu kwanza kuwa na kikosi bora kabisa, uongozi bora na usajili
bora ulio fanywa na mabingwa hao.
Ikumbukwe simba wamefanya usajili msimu huu kwa kuwachukua wachezaji wanne kutoka Azam fc akiwemo John
Bocco, shomar Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni waliopelekea wekundu hao
kupata ubingwa. Wachezaji hao wa Azam wamechangia kwa kiasi kikubwa kwa klabu
hiyo kupata ubingwa kutokana na unyumbulifu wao wakiwa uwanjani na hata mwalimu
wa timu hiyo Pierre Lechantre kuwafanya ni chaguo la kwanza kwa kila mchezo watakao cheza
katika kikosi chake.
Ni wazi kabisa Azam fc ndio waliochangia kwa kiasiki kubwa kwa
simba fc, kupata ubingwa msimu huu kutokana
na kuwa ruhusu wachezaji hao wa nne kwenda simba bila ya
kuangalia uwezo na ubunifu waliokuwa nao wachezaji hao pindi
wanapokuwa uwanjani na kuwafanya
simba kuwa na kikosi kipana
kilicho wawezesha simbakunyakua ubingwa msimu huu.
Hata hivyo ubora wao Simba auja jidhihirisha kuchukua
ubingwa msimu huu tu bali na kuwa funga wahasimu wao wajadi yanga fc, pindi walipokutana na Azam fc na
kutoa mchezaji aneongoza kwa magoli hadi sasa.
Pia simba fc imekamilisha mchakato wake na kupitisha rasmi
kwenye katiba yao mgawanyo wa hisa wa
klabu na muwekezaji. Katika mgawanyo huo
wa hisa muwekezaji ana chukua
asilimia 49 na klabu inabaki na
asilimi 51. Uku waziri mwenye dhamana na michezo Dr Mwakyembe akibariki mchakato huo.
Pia ikumbukwe Simba haijashinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania
bara tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho msimu wa 2011/12. Mpango pekee wa
Simba kwa miaka ya hivi karibuni ni kushinda taji hilo ili kurejesha heshima
Msimbazi.
Post a Comment