Ugonjwa wa Ebola wasambaa nchini DRC
Ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo sasa umesambaa kutoka maeneo la vijijini hadi mji mmoja wa eneo hilo na kuzua hofu kuwa huenda sasa ikawa vigumu kuudhibiti ugonjwa huo.
Waziri wa afya Oly Ilunga Kalenga alithibitisha kisa cha ugonjwa huo mjini Mbandaka, mji wa wakaazi milioni moja ulio kilomita 130 kutoka eno ambapo kisa cha kwanza kilithitishwa mapema mwezi huu.Mji huo ni muhumu kwa usafiri ukiwa na barabara zinazoelekea mji mkuu Kinshasa,
Watu 40 kwa sasa wameambukizwa na wengine 23 wanaripotiwa kufariki.
Ebola ni ugonjwa hatari ambao unasasabasha kufuja kwa damu ndani ya mwili na mara nyingi huua. Unaweza kusambaa kwa haraka kupitia kwa maji maji ya mwili na dalili zake hazitambuliwi kwa urahisi
Post a Comment