IFAHAMU SABABU YA EBORA KURUDI MARA KWA KWA MARA
Virusi vya Ebola vimechomoza tena, mara hii katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Wakati ni vigumu kutabiri ni wapi au lini tena mlipuko huu unaweza kuzuka, ni wazi kuwa tunafahamu mengi sasa kuhusu namna ya kuzuia janga kutokea.
Taarifa kuhusu kutokea mlipuko wa Ebola katika mji wa Bikoro kaskazini magharibi mwa Congo mara moja inaleta katika akili jinsi janga hilo linalotisha lililosababisha vifo vya watu 11,000 na wengine 28,000 kuambukizwa katika eneo la Afrika magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016.
Ni jinamizi ambalo hakuna anayetaka kulishuhudia au kulipitia tena.
Tangu Aprili 4 nchini Congo, kumeripotiwa zaidi ya visa 30 ambavyo huenda ni vya ugonjwa wa Ebola - ikiwemo vifo vya watu 18 - licha ya kwamba ni visa viwili tu vilivyothibitishwa kutokana na Ebola.
Basi ni kwanini Ebola hurudi mara kwa mara na ni jitihada gani zinazochukuliwa kuzuiwa kurudi upya kwa janga lililoshuhudiwa Afrika magharibi?
Hauwezi kudhibitiwa
Ebola unaweza kusambaa kwa kasi kupitia kugusa maji maji ya kutoka mwilini mwa muathiriwa. Dalili za kwanza zinazokuja kwa mfano wa homa sio rahisi kuzitambua.
Janga la Afrika magharibi mnamo 2014-16 lilizuka katika kijiji kimoja cha mpakani nchini Guinea, na muathiriwa wa kwanza anadhaniwa kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili aliyefariki duniani mnamo 2013.
GOOGLE
Ugonjwa huo ulisambaa nchini Guinea na nchi jirani Sierra Leone na Liberia, na kupindukia ulipofika maeneo ya mijini.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ipo maelfu ya maili kutoka mataifa ya Afrika magharibi yalioathirika na janga hilo.
Kwamba janga hilo limezuka upya katika eneo la mbali sio jambo la kushangaza.
Virusi vya Ebola vimegunduliwa katika miaka ya nyuma mnamo 1976 katika milipuko miwili ambapo watu 151 walifariki katika enoe la Nzara, Sudan kusini na watu 280 waliofariki katika eneo la Yambuku karibu na mto Ebola uliopewa jina kutokana na ugonjwa huo.
SCIENCE PHOTO LIBRARY
Mlipuko huu wa sasa unafuatia mingine 8 iliyoshuhudiwa DR Congo.
Kwa jumla kumeshuhudiwa milipuko 24 - ukiongezwa na wa kati ya 2014 -16 katika Afrika magharibi na kati ikiwemo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Uganda, Sudan na Gabon.
Wakati tunapoyatambua maeneo yalio katika hatari kubwa, itakuwa sio uhalisia kufikiria kuwa ugonjwa wa Ebola utawahi kuangamizwa kabisa na ni vigumu kujua ni wapi au lini mlipuko mwingine unaweza kuzuka.
Kutafuta kupuguza maambukizi
Tunaweza kuisitisha milipuko kuwa majanga na tunaweza kuboresha mbinu za kuwakinga raia.
Hatua ya pamoja na iliyoratibiwa katika kukabiliana na ugonjwa huu inaweza kuhakikisha ugonjwa unadhibitiwa mapema, ili watu wachache iwezekanavyo waugue au wafariki.
AFP
Ni muhimu kwanza kutambua aina ya virusi na kunakili uwezekano wa maambukizi mapya wakati mlipuko unaporitiwa.
Wataalamu kwa mfano kwa mlipuko wa sasa Congo ni lazima watambue chanzo cha maambukizi haraka iwezekanavyo.
Watataka kujua mgonjwa huyo amekuwa karibu na nani, na pia ni nani walikuwa karibu na watu hao.
Hili ni jambo linalohitaji kufanywa haraka.
Waathiriwa na wanaoshukiwa kuambukizwa watatibiwa katika taasisi za afya katika eneo hilo.
Hatua za usafi ni muhimu - ikiwemo kufuniko nyuso, na kuvaa magauni na glavu za mikono kuzuia mwili kugusa maji maji ya aina yoyote kutoka kwa muathiriwa.
Chanjo zimekusanywa
Kuna aina tano ya virusi vilivyotambuliwa vya Ebola, na kilicho hatari zaidi ni kile cha Zaire.
Na ndicho kirusi kilichotambuliwa katika mlipuko wa sasa huko Congo ambapo sasa kuna chanjo ilio tayari kwa matumizi ya dharura.
CENTERS FOR DISEASE CONTROL AND PREVENTION
Mnamo Desemba 2016, kulifanywa majaribio ya chanjo hiyo - kwa ufadhili kutoka kwa Wellcome Trust na serikali za Uingereza na Norway - imethibitisha kuwa inatoa kiwango kikubwa cha kinga dhidi ya virusi hivyo.
Iliundwa haraka wakati wa janga la mnamo 2014-16 lakini ilitoka kuchelewa kuweza kuwa na umuhimu kwa wakati huo.
Bado haijapewa kibali kamili , lakini kutokana na jitihada za kimataifa imethibitishwa kuwa salama kutumiwa kwa binaadamu na dozi laki tatu zimekusanywa.
Muhimu zaidi, wagonjwa hawatolipishwa kupokea chanjo hiyo na huenda ikafika katika eneo hilo katika muda wa kati ya siku tatuau nne.
- Chanjo ya Ebola yafanikiwa
- Guinea: Wanawake wajawazito hukwepa hospitali wakihofia Ebola
- Watu 18 waambukizwa Ebola DRC
Muongozo wa shirika la afya duniani unapendekeza kwamba iwapo kutatokea mlipuko kabla ya kibali kutolewa , chanjo hiyo inastahili kupewa kwa washukiwa wote wa ugonjwa huo, na hata wauguzi walio hatarini.
Mlipuko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo utakuwa changamoto kwa maafisa walio katika eneo hilo.
Lakini pia ni changamoto na ni fursa kwa jumuiya ya kimataifa kuthibitisha kwamba imejifunza kutokana na janga la Afrika magharibi.
Hatutarajii kuwa Ebola itapotea lakini tunaweza kutumai kuwa mbinu za kupambana zitazoeleka kiasi cha kuwa rahisi kuuzuia kwa haraka.
CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment